HATUA YA KWANZA
A) bila kuchelewa Nenda ofisi za TRA karibu na uliposema kampuni itakuwa na ofisi ili ufanye yafuatayo.
- Uchukue TIN ya kampuni (print TIN certificate)
- Ufanye makadirio ya kodi
- Upate Tax Clearance kwa ajili ya kwenda kuchukue leseni ya biashara
Hapa (ii) hakikisha umefanya makadirio kabla ya quarter husika kuisha.
Iko hivi; TRA inagawa mwaka January – December katika 4 quarters yaani
- 01 Jan-31 Mar, = First quarter
- 01 Apr – 30 June, = Second quarter
- 01 Jul-30 Sep = Third quarter
- 01 Oct – 31 Dec = Fourth quarter
Hivyo kama ulisajili January basi hakikisha unafanya makadirio kabla 31 March. Na aliyesajili tar 20 Dec hakikisha kafanya makadirio kabla ya Tar 31 Dec, YAANI KILA MTU AHAKIKISHE quarter husika aliyoanzia haipiti kabla hajaenda tra kufanya makadirio ya kodi.
ATHARI/PENALTY = kutofanya makadirio ya kodi baada ya kusajili kampuni quarter husika kupita tangu usajili inatengeneza automated penalties za 225,000
NB. Kama imetokea baada ya usajili kampuni yako kwasababu zozote za msingi haiwezi kuanza kazi basi nenda TRA wakupe mwongozo namna ya kufanya. Ila usikae kimya bila kureport, mfumo utatengeneza penalty.
B) Bila kuchelewa Jaza taarifa za Mnufaika wa mwisho wa kampuni uliyosajili (BENEFICIAL OWNER)
Beneficial Owner ni mtu yeyote mwenye mamlaka juu ya kampuni na anayenufaika na kampuni hiyo bila kujali haonekani kwenye documents za usajili au anaonekana.
Mfano A: Mtu anayemiliki kampuni lakini hataki kuonekana jina lake kwenye hiyo kampuni; hivyo anatumia watu wengine wanakuwa kama kivuli tu ila yeye ndiye mwenye mtaji na ndio yuko nyuma ya hao wanaonekana kwenye docs za Usajili na ndiye mwenye mamlaka juu ya kampuni hiyo.
Mfano B, Kama mtu wa kwenye Mfano A hayupo kwenye kampuni yako uliyosajili basi Jitaje wewe mwenyewe kuwa ndiye Beneficial owner wa hiyo kampuni uliyojiweka kuwa shareholder.
Faida za Beneficial owner utaziangalia HAPA
ATHALI/PENALTIES : Kwasasa ni 2500 kwa kila siku unayochelwa.
mfano kama Benecial owners mko wawili inamaana kwa mwezi penalty inafika 150,000 (2500x2x30= 150,000)
Pia kuna Muswada wa marekebisho kama ukianza kazi kama sheria utaofanya Penalty iwe 100,000 kwa kila Beneficial owner Plus 10,000 kwa kila siku ya ziada unayochelewa kutuma hizo taarifa.
Taarifa zinajazwa kupitia online. website ya brela. Bo.brela.go.tz
HATUA YA PILI
Nenda kachukue Leseni
- Kama leseni yako iko kwenye kundi la Class B nenda kwa afisa biashara wa seriakli wa eneo hilo anayetoa leseni/manispaa husika
- Kama leseni iko kundi la class A basi leseni hizo zinatolewa na Brela via business.go.tz
Kujua leseni ya biashara yako ni class Gani afisa biashara/manispaa wanaweza kukueleza hayo au utauliza kwa simu zilizopo HAPA
HATUA YA TATU
Tafuata CPA auditor firm, awe kama Tax Consultant wako huyo anaweza kukusaidia mambo yafuatayo
- Kukusaidia kipengele cha kwanza, na mambo yote yahusuyo TRA na kodi
- Kukupa mwongozo mzuri wa kutunza kumbukumbu za Mauzo, Manunuzi na matumizi ya kampuni yako.
- kukusaidia kuhakikisha unafanya mambo yote ya kodi kwa wakati.
HATUA YA NNE
Baada ya mwaka husika kuisha (Jan- Dec) Andaa Audited Financial Statement. hii inaandaliwa na CPA auditors waliokuwa authorized na TRA kuandaa vitabu vya mahesabu ya kampuni.
Mfano A: Kama ulisajili kampuni Tar 12 December 2021, au january au April 2021 n.k hapo inamaana kampuni ilianza mwaka 2021;
Hivyo mwaka ulipoisha 31 Dec inatakiwa iandaliwe Audited Financial statement ya mwaka 2021.
NB: HAPO HAIJALISHI KAMPUNI ILIFANYA KAZI KATIKA MWAKA HUO AU LA. Hiyo ni lazima kuandaliwa.
Hivyo kama kampuni haikufanya kazi inamaana Statement itaonesha mauzo ni sifuri.
ikishaandaliwa inatakiwa Report/annual return tumwe kwenye mfumo wa TRA ndani ya miezi sita, kuanzia Jan-June ya mwaka unaofuata.
Mfano : Financial Statement ya mwaka 2021 inatumwa mwaka 22 kuanzia Jan-June. Ndaniya Muda huo iwe imeandaliwa na kutumwa TRA.
NB: Mtu anayezituma/upload hizo taarifa TRA NI HUYOHUYO CPA AUDITOR ALIYEANDAA HIYO FINANCIAL STATEMENT kwa niaba ya kampuni yako.
ATHARI/PENALTY : Kutofanya TRA annual return filling ya mwaka uliopita ikishapita june penalty ni 225,000 kwa kila quarter unayochelewa
Mfano baada ya Jun, July – Sep ni 225,000, tena ukiendelea ikingia October – December inaongezeka nyingine 225,000, tena ikiingia january- March mwaka unaofuata inaongez 250,000 . So penalty inaendelea kuongezeka hadi siku ukisubmitt ndipo itaacha kuongezeka.
HATUA YA TANO
Baada ya mwaka mmoja Tangu tarehe kampuni yako imesajiliwa Tuma/Jaza ANNUAL RETURN YA BRELA
- kuna form inajazwa
- na unaambatanisha Financial Statement iliyoandaliwa kwenye No 4 hapo juu.
Mfano :Kampuni ilisajiliwa Brela rasmi tar 28 Sep 2021, ilipofika Mwaka 2022 kabla ya June 30 2022 uliandaliwa 2021 financial Statement na CPA auditor wako .
Hivyo ikifika Sept 28 2022 kampuni yako inakuwa imefika Mwaka mmoja tangu isajiliwa. KWAHIYO ANNUAL RETURN YA BRELA NI KUANZIA 28 SEP 2021 – 28 SEP 2022
cha kufanya ni Chukua 2021 financial statement na jaza annual return form ya brela.
ATHARI/PENALTY
Mfano : kampuni iliyosajiliwa mwaka 01/08/2019 ikachelewa kutuma BRela annual returns mpaka apofanya filling May 2022, akapewa Penalty ifuatayo
- Item 1: Late Filling Fees – 2020) – 72,000.00
- Item (2): Late Filling Fees – 20,000.00
Total Billed Amount: 92,000.00 (TZS)
HATUA YA SITA
Usisahau kufanya Renewal ya Business Lincese kwa wakati. nako kuna penalty zake kama siku zinapita baada ya license ku-expire.
Hii haijalishi unayo kampuni au la. ilimradi tu unafanya biashara na ulikuwa na leseni.
______________________________
KWA MSAADA TUWASILIANE
- 0754210627
- Bofya hapa WhatsApp
No comment